Timu ya White bird
imekubali kichapo cha mabao 2-1 walipocheza na Chwaka katika muendelezo wa ligi
daraja la kwanza taifa kanda ya Unguja hatua ya sita bora, mchezo ambao
uliovurumishwa ndani ya dimba la Amani mjini Unguja.
Katika mchezo huo ulikuwa
wa kasi kwa timu zote kwani kila timu ilitaka kupata ushindi katika mchezo huo
ili kujiwekea nafasi nzuri ya kuweza kupanda ligi kuu, ndipo Chwaka walipoanza
kuandika bao la kwanza kupitia mchezaji Ridhwan Moh’d katika dakika ya 67.
Timu hizo ziliendeleza
mashambulizi na ilipofika dakika ya 81 Bernad Lukas akaipatia Chwaka bao la
pili, lakini dakika mbili tu baada ya bao hilo White bird nao walipata bao la
kufutia machozi lililofungwa na Issa Shomari katika dakika ya 83 ya mchezo huo,na
mchezo huo ulimalizika kwa Chwaka kuondoka na alama tatu katika mchezo huo.
Akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA kocha wa timu ya
White bird Moh’d Abdul-kadir amesema kuwa,
“Mechi ilikuwa ni nzuri
bahati tu imekuwa mbaya kiupande wetu, ndo mchezo kwa sababu sisi tumetumia
nafasi tumeshindwa kuzitumia, wenzetu wametengeneza nafasi wameshinda
kuzitumia, makosa tumeyaona na tutayafanyia kazi”. Alisema kocha Abdul-kadir.
Vilevile tulizungumza na kocha wa timu ya Chwaka Issa Mjanakheir amesema
kuwa licha ya kushinda lakini mchezo ulikuwa ni mgumu.
“Mchezo mgumu lakini nimeshinda
namshukuru Mungu. Tatizo tuliloliona tutarudi mazoezini tutalirekebisha kwa
sababu mechi bado mbili kwa hiyo tatizo hulo tumeliona na tuatalifanyia kazi,
Mungu akipenda ni maandalizi tu kama tulivojiandaa mechi zote ni maandalizi tu
ili tushinde mechi nyengine”. Alisema kocaha Mjanakheir.
Matokeo hayo yameifanya
timu ya Chwaka kuwa kileleni wakiwa na alama tano (5), na White bird wao wapo
nafasi ya nne (4) na alama tatu (3)
No comments:
Post a Comment