Timu ya mabaharia weusi, Black sailors leo imewabania
Zimamoto katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya mchezo
wao wa mzunguko wa kwanza kuupoteza dhidi ya timu hiyo.

Mchezo huo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa
kumi za jioni, timu hizo zilicheza kwa kila timu kutaka kuondoka na ushindi
lakini hadi dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliyoona lango la mwenzake.
Katika mtanange huo mnamo dakika ya 66 mwamuzi Rashid
Farghan aliwatoa nje kwa kuwaonesha kadi
nyekundu mchezaji wa Black sailors Bakar Kuluzo pamoja na mchezaji wa Zimamoto
Hassan Said, baada ya kufanyiana rafu katika mchezo huo.
SALMA SPORT’S MEDIA ilizungumza na kocha wa timu ya Black
sailors Juma Awadh na akisema kuwa kukosa umakini ni tatizo la kukosa ushindi
katika mchezo wa leo.
“Tumekosa umakini hususan kwa upande wa strickers kwa hiyo mambo
ya mpira yanatokezea, tutafanya training kw asana nafikiri tukisawazisha haya
tu kila kitu kitakaa vizuri”. Alisema kocha Awadh.
Aidha kocha msaidizi wa timu ya Zimamoto, Juma Abdul-rahiim
kiupande wake amesema kuwa mchezo ulikuwa mzuri kwa timu zote.
“Mchezo ulikuwa mzuri kwa timu zote mbili, unajua timu mara
ya mwanzo ukiifunga goli nne mara ya pili itakuja kujiandaa vizuri tu, nilitegemea
tu kwamba Black sailors akija mara ya pili itakuwa shughuli nzito”. Alisema kocha
Juma.
Matokeo haya yameifanya timu ya Zimamoto kubaki nafasi ya
tatu 3 wakiwa na alama 29, na Black sailors wao wamesalia nafasi ya saba 7 na
alama 26.
No comments:
Post a Comment