Mechi za kwanza za nusu fainali za Uefa Europa League zimechezwa jana, mabingwa watetezi Sevilla wakicheza ugenini na Shakhtar Donetsk.
Matokeo ya mchezo huo
ni kwamba Timu hizo zimetoka sare ya kufungana bao 2-2 ndani ya dakika 90 za
mchezo.
Sevilla ndio walikuwa
wa kwanza kuandika bao dakika ya 6 kipindi cha kwanza kupitia kwa mchezaji
Mchin Perez, na Shakhtar Donetsk kusawazisha bao hilo dakika ya 23 kupitia kwa
Maros Romeo na Stepanenko kuongeza bao la pili dakika ya 35 kipindi cha kwanza.
Baadaye kelvin Gameiro
akaisawazishia Shakhtar Donetsk ikasawazisha bao hilo dakika ya 82 kwa njia ya
penati .
Katika mchezo mwingine
Klabu ya England Liverpool ikicheza Ugenini huko Uhispania imeambulia kichapo
cha bao 1-0 mikononi mwa Villarreal kwa bao la Adrian Lopez la dakika ya 90 ya
mchezo.
Timu zote nne zitarejeana
tena Alhamisi wiki ijayo, ikiwa ni mechi
za pili hatua ya nusu fainali.
No comments:
Post a Comment