Timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar (JKU), imezidi
kujikita kileleni mwa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya leo kuibuka
na ushindi walipocheza na Kijichi.
Katika mchezo huo uliochezwa ndani ya uwanja wa Amani, JKU
walifanikiwa kuifunga timu ya Kijichi kupitia mchezaji wake Emmanuel Martin
katika dakika ya 49 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Khamis Abdalla Terry.
Akizungumza na SALMA
SPORTS MEDIA kocha wa timu ya Kijichi Abdul Kiduu amesema kuwa mchezo
ulikuwa ni mzuri,” mchezo ulikuwa mzuri, timu imecheza vizuri lakini marifa
wajitahidi, mchezaji ata akifanya vibaya rifa hatowi, timu yetu inahakika hata
kwenye nne itaingia kwa sababu inaperform vizuri, ispokuwa mambo madogomadogo
tu, naamini game ijayo watu wataona ushindi”. Alisema kocha Kiduu.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa timu ya JKU Khamis Muhsin nae
amesema kwamba wamejipanga kwa mechi inayofuata,” tumejipanga kwa mechi
inayofuata, ushindi unashangiria ushindi wowote tu kwa hiyo point tatu tu
mezipata sie bado tunasonga mbele”. Alisema kocha Khamis.
Timu ya Kijichi licha ya kucheza vyema dhidi ya JKU katika
mchezo huo lakini walishindwa kupata bao lolote na mchezo huo ulimalizika kwa
JKU kuibuka na ushindi na kuzidi kujiweka kileleni mwa ligi hiyo.
Matokeo hayo yameifanya timu ya JKU kufikisha alama 41 wakiwa
ndio vinara wa ligi hiyo, na Kijichi wao wapo nafasi ya 12 na alama 14.
No comments:
Post a Comment