Mabao matatu ya Andy Caroll yameiiwezesha West Ham kuizuia
Arsenal na hivyobasi kuvunja matumaini ya timu hiyo kushinda taji la ligi ya
Uingereza.
Arsenal sasa ina alama
10 nyuma ya Leicester ikiwa imesalia mechi sita.
Mesut Ozil na Alexis Sanchez waliiweka Arsenal kifua mbele
kufuatia pasi nzuri za Iwobi ,lakini Caroll alifunga mabao mawili ya ghafla
ndani ya sekunde 160 ili kusawazisha.
Kichwa kizuri katika
kipindi cha pili kilimpatia Andy Caroll bao lake la tatu ,kabla ya beki wa
Arsenal Laurent Koscielny kusawazisha.
Hatahivyo West Ham iliongeza rekodi yake ya kutofungwa katika
ligi ya Uingereza na kufikia mechi 14 wakiwa nyumbani ,lakini kikosi hicho cha
kocha Slaven Bilic kinasalia nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya Uingereza.
No comments:
Post a Comment