Ligi kuu ya soka ya England imeendelea tena jumapili kwa
michezo mitatu ,Sunderland wakicheza nyumbani dhidi ya vinara wa ligi Leicester
city, waliambulia kipigo cha mabao 2-0, na kuwafanya leicester city kufikisha
alama 72 katika Msimamo.
Liverpool waliibamiza stoke city kwa kichapo cha mabao 4-1
yaliyofungwa na wachezaji Alberto Moreno, Daniel Sturridge na Divock Origi
(mabao mawili) huku bao pekee la kufutia machozi la Stoke City likifungwa na
Bojan Krikic.
Na Mechi ya tatu ya mwisho kati ya Tottenham na Manchester
united mchezo ulimalizika kwa United kuchabangwa mabao 3-0.
Dakika ya 70 mchezaji Dele Alli alianza kuiptia goli bao la
kwanza Tottenham .
Tottenham iliandika bao la pili kupitia kwa Toby
Alder-weireld, huku bao la tatu likipachikwa na Erick Lamela dakika ya 76.
No comments:
Post a Comment