Katika mtanange huo
kila timu ilikuwa inataka kuondoka na alama tatu muhimu ili ziweze kuwaweka
katika hatua nzuri ya kutinga nne bora kwa upande wa Unguja ili waweze kucheza
katika kinyang’anyiro cha kuweza kulinyakuwa kombe la ligi hiyo.
Timu hizo licha ya
kucheza vyema lakini hadi mtanange huo unamalizika hakuna timu ambayo imeona
lango la mwenzake na hivyo kufanya kugawana alama katika mtanange huo.
Black sailor sasa
wameshacheza mchezo 22,wakiwa na alama
34 na wanakamata nafasi ya sita 6, wakati na Miembeni pia wameshacheza michezo
22,wakikamata nafasi ya saba 7, na alama zao ni 31 katika msimamo wa ligi kuu
ya Zanzibar kanda ya Unguja.
Mpaka sasa ukiachana na
JKU ambayo ina nafasi kubwa ya kuingia nne bora kwa Unguja,lakini timu tatu nyengine
bado ni ngumu kuzijua ambazo zitaungana na JKU katika kinyang’anyiro hicho
kutokana na alama walizonazo na jinsi marokeo ya mechi zao yanavyokuwa.
Ukiangalia msimamo wa
ligi kuu ya Zanzibar kanda ya unguja JKU wana alama 50, Mafunzo alama 39,
Zimamoto 36, KMKM,KVZ na Black sailors wote wana alama 34,Miembeni alama 31,
Kipanga wa alama 30, Kimbunga alama 26,Jang’ombe boys alama 25, Chuoni alama
24,Kijichi wana alama 18, Polisi alama 14 na Mtende wana alama 10.
Kutokana na msimamo huo
hakuna timu ambayo utaihesabu moja kwa moja katika kuelekea hatua ya nne bora.
No comments:
Post a Comment