Wasimamizi wa Ligi ya Uhispania wanapanga kuanza kuadhibu klabu ambazo zitaruhusu viti visivyo na mashabiki kuoneshwa kwenye runinga.
Hilo litaanza kutekelezwa
kuanzia msimu ujao.
Kanuni mpya zinazitaka
klabu za ligi kuu kuhakikisha maeneo yanayoangaziwa na kamera za runinga
yamejaa mashabiki.
Lengo la hatua hii ni
kuhakikisha viwanja vinavutia zaidi kwa watazamaji na pia kuongeza ushindani wa
La Liga dhidi ya Ligi Kuu ya Uingereza.
Mei 2015, Uhispania
ilipitisha sheria mpya za kuwezesha haki za kupeperusha mechi kuunganishwa na
kuuzwa pamoja kama fungu moja.
Awali, klabu kama vile
Real Madrid na Barcelona zilikuwa zikijitetea kivyake na kupata mikataba ya
thamani kubwa.
bbc.
No comments:
Post a Comment