
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo yuko sawa kuchezea klabu yake dhidi ya Manchester City katika mechi ya nusufainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mechi hiyo ya marudiano
itachezewa Santiago Bernabéu kuanzia saa nne kasorobo usiku. Mechi ya kwanza
ilimalizika 0-0.
Ronaldo, ambaye
amefunga mabao 93 mechi za Ulaya, hakuweza kucheza mechi ya mkondo wa kwanza
kutokana na jeraha misuli ya paja.
"Cristiano yuko
sawa, 100%. Alishiriki mazoezi leo na atakuwepo kesho,” meneja wa Real Zinedine
Zidane alisema Jumanne.
Kiungo wa kati wa City
Yaya Toure, ambaye pia alikosa mechi ya kwanza kutokana na jeraha alifanya
mazoezi Jumanne pia.
Kiungo wa kati Samir
Nasri, mshambuliaji David Silva na beki Pablo Zabaleta wote hawatarajiwi
kuchezea City.
Meneja wa Manchester
City Manuel Pellegrini amewatahadharisha wachezaji wake kumhusu Ronaldo.
"Cristiano daima
atasalia kuwa mchezaji tofauti. Hufunga mabao mengi na amekuwa akifanya hivyo
miaka yote sita ambayo amekuwa hapa,” amesema Mchile huyo aliyekuwa mkufunzi wa
Real klabu hiyo ilipomnunua Ronaldo.

Pellegrini anaamini
Aguero atawatatiza walinzi wa Real Lakini ameongeza kusema: "Sidhani Real
ni Cristiano Ronaldo pekee. Lazima tufanye bidii kama timu kujilinda na
kushambulia. Sio dhidi ya Ronaldo pekee lakini dhidi ya Real Madrid."
Amesisitiza pia kwamba
klabu hiyo ya Uhispania pia itakuwa na kibarua kudhibiti washambuliaji wa City,
akimtaja Sergio Aguero aliyefunga mabao 28.
Aguero alipumzishwa
mechi ambayo City walilazwa 4-2 ugenini Southampton Jumapili.
Upande wa Real, bado kuna
shaka kumhusu Karim Benzema.
Kiungo wa kati wa
Brazil Casemiro aliumia kidogo wakati wa mechi ya La Liga Jumamosi ambayo
walishinda 1-0 ugenini Real Sociedad lakini anatarajiwa kukabili City.
Mshinid atakutana na
Atletico Madrid kwenye fainali 28 Mei mjini Milan. Atletico waliwaondoa Bayern
Munich nusu fainali.
No comments:
Post a Comment