
Timu ya Mtende rangers imezidi kuyumba katika ligi
kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kuchezea kichapo cha mabao 2-0 walipocheza na mabaharia
weusi timu ya Black sailors katika mchezo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani
mjini Unguja.
Mabao ya Black sailors yamefungwa na Mustafa Vuai katika
dakika ya 27, na Abdul-Aziz Hassan dakika 37.
Mtende walionesha kiwango kizuri na wameweza
kuutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa lakini walikosa mabao mengi katika
mtanange huo, licha ya kucheza vyema lakini Mtende walimaliza mchezo bila ya
mafanikio yoyote, kwa kufungwa kwa mabao 2-0.

Mtende bado wanaburuta mkia wakiwa na alama kumi 10,
na Black sailors wao wapo nafasi ya saba 7 na alama 29.
No comments:
Post a Comment