Bado tunaendelea na kampeni yetu hii, lengo kuu ni kuwafichua
na kuwaonesha wanamichezo wadogowadogo ambao wanaaminika kua wanavipaji vya
hali ya juu katika michezo, iwe mpira wa miguu, mchezo wa ngumi, mpira wa
kikapu nk.
Kampeni yetu hii ipo katika mokoa yote ya Unguja na Pemba , tafadhali
shiriki nasi katika kampeni hii kuibua vipaji vya vijana wetu, inaonekana
vijana vipaji wanavyo lakini vinashindikana kuonekana hadharani.
Kwa yoyote mdau wa michezo ambae anatimu ya watoto ya mchezo
wowote au hata kijana pekee unaomba kuwasiliana
nasi kupitia +255779518500 /
salmahassan040@gmail.com tujadiliane ni namna gani ya kuwafikia vijana wetu au
wewe mwenyewe na tuandae mbinu mbadala za kuwatangaza.
Picha uzionazo ni wanafunzi wa Skuli ya Ng'ambwa visiwani Pemba hapo wanafanya mazoezi ya mpira wa NETBALL
wakijitayarisha na sherehe za michezo ya elimu bila malipo Zanzibar nje ya
uwanja wa wa Gombani.
No comments:
Post a Comment