Friday 6 May 2016

Mmiliki wa Timu ya TP Mazembe Atangaza Kuwania Urais Jamhuri ya Demokrasia ya Congo


MOISE Katumbi Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga, Mkurugenzi wa klabu ya TP Mazembe na mfanyabiashara marufu nchini Kongo ametangaza kugombe urais wa Novemba mwaka huu.

Muungano wa vyama kadha vya upinzani umemuidhinisha Katumbi kuwa mgombea huku muungano huo ukiwa umegubikwa na hofu ya huenda Rais Joseph Kabila akaendelea kushikiri madaraka kinyume na katiba hiyo.

Katumbi amekuwa Gavana wa jimbo la Katanga tangu 2007 chini ya chama cha People’s Party for Reconstruction and Democracy(PPRD) na baadae akajiuzulu nafasi hiyo septemba 2015 ambapo mwaka huu 2016 amekuwa akitoa kauli zinazo mtaka Kabila kuheshimu katiba ya taifa hilo inayo mtaka kustaafu mwishoni mwa mwaka huu.

Licha ya Katumbi kumsaidia Kabila katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2006 na 2011 kwasasa anaonekana kuwa mbali na kiongozi huyo tangu kujiuzulu kwake 2015.

Hata hivyo mfanyabiashara huyo amekuwa na umaarufu mkubwa kutokana na kumiliki klabu ya TP Mazembe tangu 1997.

Uchaguzi huo unaonekana kuwa na mchuano mkali kwa kuwa Katumbi ana nguvu kubwa ya kiushindani kuanzia katika jimbo la katanga na katika ngazi ya taifa licha ya kukabiliwa na tuhuma za ubadhilifu wakati wauongozi wake.



Wachunguzi wa habari za siasa wamesema nchi hiyo inanyemelewa na machafuko iwapo Rais Kabila atataka kuendelea kuongoza taifa hilo kwa nguvu kama ilivyo fanyika Burundi na Rais Nkurunzinza.

No comments: