Tuesday 10 May 2016

KIMBUNGA YABAMIZWA 3-1 LIGI KUU YA ZANZIBAR.



Timu ya Kimbunga imepokea kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa wanajeshi wa Kipanga katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa ndani ya uwanja wa Amani mjini Unguja.
Katika mchezo huo Kipanga walicheza kwa kasi na wakafanikiwa kufunga bao la kwanza baada ya mchezai Mukhdhar Ahmada kupachika kamba kali hadi wavuni katika dakika 25.

Mnamo dakika ya 42 Daud Nyerere akaipatia Kipanga bao la pili, na Mukhdhar Ahmada akarudi tena kwa kupachika bao la tatu katika daika ya 57.

Kwa upande wa bao la kufutia machozi la Kimbunga limewekwa kambani na Khamis Muhidin mnamo dakika ya 83 ya mtanange huo.

Kipanga sasa wamefikisha alama 27, wakiwa nafasi ya nane 8 na Kimbunga wapo nafasi ya kumi na alama 23.

No comments: