
Timu ya Polisi bado ipo katika wakati mbaya katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya leo kuupoteza mchezo wake walipocheza na Zimamoto kwa kucharazwa mabao 2—0.
Katika mchezo huo
uliosukumwa majira ya saa kumi za jioni ndani ya dimba la Amani, mabao ya
Zimamoto yamewekwa kambani na Hakiim Khamis katika dakika ya 43 na 64.
Polisi wameshinda
mchezo mmoja tu tangu kuanza kwa ligi hiyo katika michezo takriban 19
waliyocheza na sasa wana alama 10 katika msimamo wa ligi hiyo.
Zimamoto wao wapo
nafasi ya tatu 3 wakiwa na alama 32 katika msimamo wa ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment