
Dereva Lewis Hamilton
anahofia matatizo ya kutokuaminika kwa injini ya ya gari analolitumia kuwa
inaweza kuwa sababu ya kutomfikia hasimu wake anayetumia gari la Mercedes Nico
Rosberg.
Hamilton yupo alama 43
nyuma ya Rosberg baada ya kumaliza wa pili katika michuano ya jana jumapili ya
Russian Grand Prix. Muingereza huyo alisema'' wasiwasi wangu sio kumshinda
Nico.Wasiwasi wangu ni iwapo nitaweza patiwa gari litakalonifanya nishindane
sawasawa.''
"Je, haitaweza
kutokea tena? Hapana kutakuwa na matatizo mbeleni." Sikia: 'Hali ya kukata
tamaa inaanza kumkumba Hamilton'Maneno ya Hamilton yanaashiria mlolongo wa
matatizo ambayo yamekuwa yakimkumba katika michuano miwili iliyopita.

Nchini Urusi,kufeli kwa
injini kulimfanya akamaliza akiwa nambari kumi.Baadaye alijaribu tena kupambana
zaidi na kushika nafasi ya pili baada wataalamu wa gari lake walilifanyia
marekebisho usiku kucha.
Wiki mbili zilizopita
nchini China pia alikumbwa na tatizo la injini na kumfanya ashindwe kushiriki
vizuri,akimaliza nafasi ya saba huku gari lake likiishia kuharibika.
Alianza pia vibaya
katika mashindano mawili tofauti nchini Australia na Bahrain yaliyomfanya
kuishia nambari mbili na tatu.Rosberg ameshinda katika mbio zote nne
alizoshiriki msimu huu.
No comments:
Post a Comment