Tuesday, 3 May 2016

SAMUEL ETO’O AZIDI KUJIJENGEA SIFA KWENYE LIGI NCHINI UTURUKI

Samuel Eto’o azidi kujijengea sifa kwenye ligi nchini Uturuki

Nyota wa Cameroon Samuel Eto’o akimbizana na Mario Gomez kwenye kinyang’anyiro cha mfungaji bora.

Mshambuliaji wa Cameroon Samuel Eto’o anayechezea kilabu ya Antalyaspor nchini Uturuki, anaendelea kujijengea sifa kwenye ligi kuu ya soka ya Super Lig Spor Toto.

Eto’o ameonyesha umahiri wake kwa kufungia  Antalyaspor jumla ya magoli 20 kwenye ligi katika mechi 31 zilizochezwa.


Kufuatia mafanikio hayo, Eto’o anaendelea kukimbizana na mshambuliaji wa Ujerumani Mario Gomez anayechezea kilabu ya Beşiktaş na ambaye kwa sasa amefunga jumla ya magoli 24.


Msemaji wa kilabu ya Antalyaspor Hasan Ali Ceylan alibainisha umuhimu wa Samuel Eto’o kwenye timu hiyo na mchango wake mkubwa alioleta katika mafanikio yao.


Vile vile, Ceylan pia alifahamisha kwamba mchezaji huyo atapokea malipo ya ziada kufuatia makubaliano yao ya mkataba kwa kuifungia magoli 20.

 

No comments: