
Klabu ya soka ya Leicester City wameshinda taji la ligi kuu England katika historia inayovutia kwenye ligi hiyo. Suluhu ya 2-2 waliyoipata Tottenham dhidi ya Chelsea siku ya jumatatu usiku ilisababisha mafanikio hayo makubwa kuwahi kutokea kwa upande wa Claudio Ranieri.
Leicester walianza
kampeni zao za ubingwa huku wakipewa nafasi moja tu kati ya 5000 kushinda taji
la ligi na pia wakitoka katika janga la kutaka kushuka daraja.

Lakini wamepoteza
michezo mitatu tu katika kile kinachotafsiriwa kama hadithi za kale na ushindi
wa kipekee katika timu hiyo. Wapinzani wao wa karibu Spurs,Arsenal,Manchester
City, Manchester United na washindi wa ligi msimu uliopita Chelsea wameshindwa
kuwazuia mbweha katika msimu mzima wa ligi.

Leicester City ni
mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza mara ya kwanza kabisa
5,000-1 uwezekano wao
wa kushinda ligi msimu ulipoanza
2-2 matokeo ya mechi
kati ya Chelsea na Tottenham ambayo iliwazawadi Leicester taji la ligi
''Kwa kigezo cha soka
la ndani,Leicester City kushinda taji la ligi kuu ni mafanikio makubwa sana
katika historia na haiwezi kusahaulika'' kiungo wa zamani wa Leicester Robbie
Savage ameiambia BBC.''Ni jambo la ajabu.Hii ni hatua ya mageuzi katika
historia ya Ligi Kuu."
Rais wa shirikisho la
soka duniani Gianni Infantino amesema historia nzuri ya Leicester ilikua ni
kama hadithi za kale.
No comments:
Post a Comment