Tuesday 17 May 2016

Serena na Murray ndio mabingwa wa Internazionali BNL d'Italia



Jamvi la mashindano ya tenisi ya Internazionali BNL d'Italia lilikunjwa hapo jana baada ya fainali kuchezwa kwa upande wa wanawake na wanaume.

Kwa upande wa wanawake, mwanatenisi nambari 1 duniani Serena Williams alimshinda Madison Keys seti 2-0 za msururu wa 7-6 na 6-3 na kutawaza bingwa wa taji hilo.

Serena amefanikiwa kushinda taji hilo kwa mara ya 4 baada ya kuwahi kushinda mwaka 2002, 2013 na 2014.

Na katika upande wa wanaume, mwanatenisi nambari 1 duniani Novak Djokovic alishindwa kutamba mbele yaAndy Murray.

Murray alinyakuwa ubingwa wa  taji hilo kwa kumcharaza Djokovic seti 2-0 za msururu wa 6-3 na 6-3.

No comments: