Friday 17 June 2016

Sturridge aokoa England Euro 2016.

Daniel Sturridge alifunga bao dakika za mwisho na kuwasaidia England kuondoka na ushindi muhimu katika Kundi B michuano ya Euro 2016.
Huo ulikuwa ushindi wao wa kwanza katika fainali hizo zinazochezewa Ufaransa.
Kipa Joe Hart alibabaisha na kuwezesha Gareth Bale kufunga frikiki akiwa hatua 30 kutoka kwenye goli kipindi cha kwanza na kuwaweka Wales kifua mbele mechi hiyo iliyochezewa Lens.
Wachezaji wa Roy Hodgson walizomewa wakiondoka uwanjani kwenda mapumziko na ilikuwa bayana kwamba hatima yake kama kocha ilikuwa kwenye mizani.
Lakini aliwaingiza uwanjani Jamie Vardy na Sturridge kipindi cha pili nafasi za Raheem Sterling na Harry Kane.


Vardy alisawazishia England dakika ya 56.
England waliendelea kushambulia na dakika za mwisho Sturridge alimbwaga kipa Wayne Hennessey na kuwezesha timu yake kuondoka na ushindi wa 2-1.
England wanaongoza Kundi B na wanahitaji alama moja kutoka kwa mechi yao dhidi ya Slovakia Jumatatu kufuzu kwa hatua ya 16 bora.
Wales watahitaji kulaza Russia ndipo wamalize wakiwa nafasi mbili za kwanza.
bbc

No comments: