Sunday 28 February 2016

DOGO RASHFORD AIPIGIA MBILI MAN UNITED IKIICHAPA 3-2 ARSENAL, UINGEREZA



Mshambuliaji kinda wa miaka 18 wa Manchester United, Marcus Rashford akiruka juu kushangilia baada ya kuifungia timu yake mabao mawili dakika ya 29 na 32 katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Arsenal kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza jioni ya leo Uwanja wa Old Trafford. Bao lingine la Mashetani Wekundu limefungwa na Ander Herrera dakika ya 65, wakati ya Washika Bunduki wa London yamefungwa na Danny Welbeck dakika ya 40 na Mesut Ozil dakika ya 69.

No comments: