Monday 14 March 2016

AMANI FRESH YAICHAPA WEST COAST 1-0.


Katika mchezo wa ligi daraja la pili wilaya ya Mjini uliosukumwa jana ndani ya dimba la Amani mjini Zanzibar, timu ya West coast imekubali kichapo cha bao 1-0 walipofungwa na Amani Fresh.
 
Mtanange huo uliosukumwa majira ya saa nane za mchana, timu zote zilifanya mashanbulizi ya mara kwa mara, pia zilipata nafasi za kushinda lakini nafasi hizo hawakuzitumia vyema.
 
Bao pekee la Amani Fresh limewekwa kimyani na mchezaji Rashid Suleiman katika dakika ya 50 ya mchezo huo.
Baada mchezo huo SALMA SPORT MEDIA ilizungumza na kocha wa timu ya West coast Issa Ramadhan ili kutaka kufaham kipi kilichopelekea timu yake kufungwa katika mchezo huo, Kocha Issa amesema walipata nafasi lakini wameshindwa kuzitumia.
“Tumepata nafasi lakini tumeshindwa kuzitumia na wenzetu wamezitumia ilo limekuwa tatizo la kila siku, ni umakini tu kwa sababu kila siku tunafahamishana icho kitu lakini cjui tufanye kitu gani zaid ili wapate kutufaham, nafikiri ni kufanya mazoezi ya kufunga zaidi tutaendelea kufanya labda nafikiri wanaweza wakabadilika tunategemea hivyo”. Alisema Kocha Issa.
Vile vile kocha wa timu ya Amani Fresh Said Hakiim Suleiman amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri kwa timu zote lakini Allah amewaajalia kushinda wao katika mchezo huo.
“Mchezo ulikuwa ni mzuri na wa nguvu wachezaji wamejitahidi wa pande zote mbili ispokuwa Allah ametujaalia sisi kushinda, tutatakaa pamoja ili kuyashughulikia makosa mazoezini, tumebakisha game mbili na kwa uwezo wa Allah tutaingia katika ya nane 8 bora”. Alisema kocha Said.
 Katika mtanange huo timu ya Amani Fresh wamevaa jezi rangi ya kijani na West coast wamevaa jezi rangi ya blue.
Katika mtanange huo timu ya Amani Fresh wamevaa jezi rangi ya kijani na West coast wamevaa jezi rangi ya blue.

No comments: