Sunday 13 March 2016

TIMU YA BARCA BADO YAENDELEA KUTESA


Barcelona imeendelea kufanya yake kwenye La Liga na kuizabua Getafe kwa bao 6-0 kwenye uwanja wa Nou Camp siku ya Jumamosi wakati Luis Suarez, Ivan Rakitic na Dani Alves wote wakiwa benchi wakiangalia pambano hilo.
Goli la kujifunga la mapema la Juan Rodríguez lilianza kuonesha dalili kwamba Getafe watafungashiwa zigo la magoli.
Dakika tatu baadaye, Leo Messi alikosa penati ambayo iliokolewa na golikipa Guaita. Hiyo ilikuwa ni penati ya 8 kupotezwa na Barcelona katika msimu huu.
Messi alipika bao ambalo liliwekwa kambani na Munir na kuiandikia Barcelona bao la pili dakika ya 19 na dakika ya 32 mu-argentina huyo alipika bao jingine Neymar akweka kambani.
Dakika nne baadaye kabla ya mapumziko, Messi akatupia bao la nne kwa shuti kali akiwa nje ya box.
Neymar alipachika bao lake la pili kwenye mchezo huo kwa msaada mwingine kutoka kwa Messi na kufanya matokeo kuwa 5-0 kabla ya Arda Turan kukamilisha ushindi kwa bonge la bao.

No comments: