Friday 11 March 2016

EL-HILAL WAIBUKA NA USHINDI WA MABAO 2-1



Timu ya El-hilal leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 walipo wafunga Gulioni katika mchezo wa ligi daraja pili wilaya ya mjini uliosukumwa ndani ya dimba la Amani hapa visiwani Zanzibar.

Mchezo huo uliochezwa majira ya saa nane za mchana, timu ya El-hilal walikuwa ndio wa mwanzo kuliona lango la wenzao baada ya mchezaji wake Ussi Ali, lakini Gulioni wakafanikiwa kusawazisha kupitia mchezaji Abdul-Aziz Janu.

Timu hizo zilicheza mpira wa kuvutia na pia zilikosa nafasi nyingi za kufunga, lakini mchezaji wa El-hilal Ali Said, ndipo aliposawazisha makosa yaliyojitokeza kwa wachezaji wenzake baada ya kuupiga mpira kwa kichwa na kuingia nyavuni moja kwa moja, na kuyafanya matokeo kuwa mabao 2 kwa 1.

Kocha wa timu ya Gulioni Fahmi Dego amesema kuwa mchezo ulikuwa ni mzuri
“mchezo ulikuwa ni mzuri,lakini kama kuna hujuma tunayofanyiwa timu
ya Gulionibasi hujuma hizo zitafeli,kuna watu wanaihujumu hii timu lakini inshaallah kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu hii timu itakwenda vizuri tu, na hizo hujuma zao zitakwisha”. Alisema kocha Dego.

Aidha aliendelea kwa kusema “wapenzi wangu na mashabiki watulizane, leo tumefungwa tunajipanga zaidi”.

Kwa upande wake Nahodha wa timu ya El-hilal, Ismail Salum amesema kwamba mchezo ulikuwa ni mzuri lakini hakuacha kutoa malalamiko juu ya waamuzi

“mchezo ulikuwa ni mzuri japo kuwa marifa hawapo makini,na  viongozi wa mpira wanawaona,wahusika hawapo makini, lakini wangekuwa wapo makini na wanalifatilia hili jambo basi lingekuwa tayari  washalitatua”. Alisema Ismail.


Timu ya El-hilal ikiwa imeavalia jezi rangi nyekundu, na Gulioni wamevaa jezi rangi nyeupe kwa blue bahar.

No comments: