Wednesday 24 February 2016

Ghana kuandaa mashindano ya Marathon kwa ajili ya amani


Ghana imezindua mpango wa maandalizi ya mashindano ya Millennium Marathon ya amani barani Afrika yatakayoanza tarehe 3 mwezi Septemba mwaka huu.
Mashindano hayo yatakayobeba kauli mbiu ya ''Afrika Ipo Mbioni'', yanalenga kuzindua jamii za Afrika kuhusu umuhimu wa amani, utulivu na afya bora.
Mashindano hayo yatashirikisha wanariadha zaidi ya 40,000 kutoka Afrika na kimataifa.
Mshindi wa mashindano hayo ya marathon ya mwaka huu ataondoka na kitita cha fedha dola 150,000.

No comments: