Soka la Tanzania limesemwa kua
ni shida kukua kutokana na kutokuwepo
kwa mpangalio mzuri wa kuwezesha wachezaji na soka lenyewe ili kulikuza.
Kauli hiyo imetolewa na Yunus
Dady wa timu ya “Bhulyanhulu” ya Shinyanga
inayo cheza daraja la pili
kugombania kufuzu ligi daraja la kwanza wakati alipokua akizungumza na SALMA
SPORT’S MEDIA juu ya mtazamo wake kwa soka la Tanziania.
Mengi ameyaongea mchezaji huyo na katika
maongeziyetu ilikua kama ifuatavyo:-
Salma Hassan: unalizungumziaje
soka la Tanzania kwa ujumla?
Dady: mpira wa Tanzania kiufupi ni mgumu na wanaofanya uwe mgumu ni
baadhi ya viongozi.
Salma Hassan: oky sawa , kivipi
unakua mgumu au awo viongozi wanaufanya vipi kua mgumu?
Dady: kwamfano utakuta mtu
anacheza timu kubwa hapa nchini lakini
inafikia hatua mchezaji miez mitatu (3) mapaka mine(4)hajapewa mshahara wake hivi unategemea mchezaji kama
huyu anaweza kumentain pafomance yake wakati maisha yetu haya tunayajua wenyewe
! lakini ni tofauti kabisa na wenzetu wa Ulaya wanajali , wanathamini na wanajua
kuvienzi vipaji na wachezaji.
Salma Hassna: kama hali ndio hiyo
uliyoieleza ni kweli mchezaji anaweza kurudi nyuma kutokana na mazingira mabovu
kama hayo kulinganisha na maisha ya wengi hapa nchini ni “duni” kwa uwoni wako
nini kifanyike ili kuinua soka letu ?
Dady: kitu cha kwanza viongozi
waache ubabaishaji, kwa sababu Tanzania na timu zake wanavipaji vingi sana lakini viongozi wanaviua wenyewe eti
huwez kucheza Primier ligi mpaka
upate mtu wa kukusimamia na awe anakupigia debe ucheze hata uwe na kipaji gani
lazima awepo mtu awe na sauti juu yako wa kukusimamaia la sihivyo huwez kupata
nafasi ya kucheza na utaishia patupu! na mifano ipo mingi, sasa hivi kuna watu
wapo vijijini wanauwezo mkubwa lakini ndio hivyo wanaachwa na pia Sponser
(wadhamini )hawana sasa watafanya nini.
Yunus Dady amemalizia kwa kutoa
wito kwa viongozi wote wa soka nchini kua makini na kujali kipaji na uwezo wa
mchezaji lakini pia kuzingatia maslahi ya mchezaji wenyewe,wawezeshwe ili nao
wapate moyo kwa kucheza kwa bidii na hatimae kukuza soka letu hapa nchini.
Dady ni mchezaji machachari nae valia
jez nambari 5 mgongozi na
uwanjani anachezea beki wakati nambari
tano 5.
1 comment:
ni kweli kabisa viongozi huwa wanajali maslahi yao zaidi
Post a Comment