Mashabiki na wadau wa soka nchini
wamesema kua soka la Tanzania bado lipo katika kiwango cha chini na si cha
kurisha kutokana na mfumo mbaya wa uwendeshaji wa soka hilo.
Wamesema kua ukiachana na
viongozi , timu zenyewe zimekosa misingi bora ya kuibua vipaji vyao wenyewe
kutokana na utaratibu wa kufikiria kwa upana juu ya ukuzaji wa soka kutokuwepo.
Mmoja miongoni mwa wadau hao
Najeli Kihongosi kutoka Iringa aliezungumza na SALMA SPORT’S MEDIA juu ya
mtazamo wake katika soka la Tanzania.
Kihongosi amekiri kwa kusema ni kweli soka la hapa nchini ni chini ya
kiwango na itachukua muda kukua, ametolea mfano kwa kusema vilabu vingi hapa nchini havina Academy za
kukuza vipaji ,hawana viwanja vyao
wenyewe lakini pia uongozi wa TFF haujasimamia uanzishwaji wa Academy kwa kila
kilabu.
Amesema kama TFF wangeweza
kusimamia hili la uwanzishwaji wa Academy basi nchi ingekua na kutajika pakubwa
kwa soka.
Aidha amesema changamoto nyingine
ni uchumi hafifu kwa vilabu vingi hapa nchini kiasi ambacho wanashindwa
kuyafikia malengo yao waliojipangia kutokana na kua na uchumi mdogo.
Kwa upande mwengine Kihongosi
ametoa wito kwa wadau na wanasoka nchini kwa kusema, timu kubwa na kongwe kama
Simba na Yanga na nyenginezo ni lazima wawe na viwanja vyao kwani wana
rasilimali watu wengi kuzisaidia timu zao.
Pia amesema, timu za mikoani
zitafute udhamin ili wajengewe viwanja na wadhamini nao pia wajitokeze
kudhamini timu hizo kwani zitakapoweza kua na Academy hizo zitazalisha vipaji
vya hali ya juu.
Halkadhalika ameitaka TFF
ihakikishe inasimamia sheria za mapato ili kuwa na uchumi imara huku ikihakikisha
mianya yote ya uchakachuaji wa ticket unakomeshwa pia itafute udhamin
imara ili timu ziwe 20 ligi kuu na kuboresha ratiba kuepusha upangaji matokeo
na kupata kilichobora.
1 comment:
Big up Salma
Post a Comment