Monday 29 February 2016

MTIHANI WAMFANYA RASHFORD ASHINDWE KUSHEREKEA USHINDI DHIDI YA ARSENAL



Msahau kabisa Anthony Martial kuna kipenzi kipya pale Old Trafford kwa sasa
Kinda wa Manchester aliyepandishwa kwenye kikosi cha wakubwa Marcus Rashford amekuwa na wiki nzuri baada ya kufunga magoli mawili katika mchezo wa Europa dhidi ya Midtjylland lakini pia alifanikiwa kufunga magoli mengine mawili dhidi ya Arsenal jumapili hii.
Goli 4 katika mechi mbili ni wastani mzuri kwa kinda huyo utakaompa ujasiri wa kufikia mafanikio mengine mengi tu.
Kinda huyu ni wazi ana kipaji cha hali ya juu cha kumfanya kuja kuwa moja ya wachezaji wakubwa duniani, lakini katika umri wa miaka 18 tu Uongozi wa Manchester United lazima ufanye kila liwezekanalo kuhakikisha Rashford anaendelea kuwepo Old Trafford kwa miaka mingi ijayo.
Pamoja na yote hayo Rashford bado ni Mwanafunzi na ana vitu vingi sana kama tahadhari
Alipoulizwa na Mwandishi wa Habari kama ataenda kusherehekea Ushindi dhidi ya Arsenal alijibu kuwa Hawezi kwa sababu kesho atakuwa na mtihani wa Chemistry.

No comments: