Wadau
na wachezaji wa soka nchini wamelalamikia juu ya ukuaji wa soka nchini wakisema
kiwango cha ukuaji wake hakiridhishi kabisa na kwamba juhudi kubwa inahitajika
kufanyika.
Wamesema,
kadiri ya siku zinavyosonga mbele badala ya kwenda mbele ndio kiwango
kinavyorudi chini ingawa katika hali ya
juujuu kinaonekana kukua lakini sio uhalisia wenyewe.
Wakiongea
na SALMA SPORT’SMEDIA kwa nyakati tofauti wadau wa soka nchini wameonesha
kutoridhidhwa na mazingira ya uchezeshwaji wa ligi wakisema umejaa mapungufu
ndio sababu kuu inayo pelekea kutokukua kwa soka la Tz kasi zaidi.
Mmoja
miongoni mwa waliokua wachezaji walioichezea timu ya Mvomerou wiliya, timu ya Morogoro katika ligi ya kill taifa
Cup na Police Morogoro ligi daraja la
kwanza msimu wa 2014 -2015 Salumu Juma amesema kutokana na uwendeshaji mbovu wa
ligi za tz inapelekea timu nyingi kutopiga hatua mbele “soka la Tz ukuaji wake
hauridhishi kwa kiasi kikubwa na hili linatokana na uwendeshwaji wake mbovu wa
ligi zetu”alisema Juma.
Amesema
waamuzi wanafanya maamuzi yao binafsi na bado wapo wanaendelea na kazi zao hali
ambayo inarudisha nyuma na inakatisha juhudi za wachezaji.
Akitoa
mchango wake juu ya nini kifanyike ili kukuza soka letu ameiomba TFF iboreshe ligi za daraja la kwanza kwani ndio
zinazoonesha vipaji vya wachezaji kwa haraka sana pamoja na kuwaandaa vizuri
waamuzi wa michezo hiyo.
Pia
ameishauri TFF ianzeshe vituo vingi vya
soka nchini kwaajili ya watoto kwani wengi wanajitihada kucheza soka lakini
wanashindwa na wapi pakukimbilia, amesema kufanya hivyo kutasaidia kuibua
vipaji katika nchi yetu.
Nae mildifild na mshambuliaji wa timu ya Ruvu
shooting ligi daraja la kwanza Mkoa wa
pwani Ayoub Kitala akizungumzia juu ya
changamoto zinazolikabili soka la Tanzania amesema kitu kikubwa kinachochangia
soka kushuka ni waamuzi wasiozingatima maadili ya kazi zao “soka la bongo
marefa ndo wanaosababisha soka lichelewe kukua haraka kwa sababu wengine
wanachezesha huku wakiwa na yao moyoni”alisema Kitala
Amesema
waamuzi wengi katika uchezeshaji wao wanazibeba timu ambazo hazina uwezo hali ambayo imeelezwa kua
kufanya hivyo huko mbele ndio kunakua na timu kubwa mbovu.
No comments:
Post a Comment