Chama cha Judo Zanzibar kinatarajia kuwa mwenyeji kuandaa
mashindano 11 ya Judo ya Afrika Mashariki na Kati ambayo yanatarajiwa kufanyika
mwanzoni mwa mwaka 2017.
Taarifa hizo zimethibitishwa na Makamu Urais wa shirikisho la
Judo Afrika Mashariki na Kati Yussuf Thabit Mbalambula alipozungumza nasi leo
hii.
Mbalambula amesema baada ya kufanya kikao chao kwenye
shirikisho lao wameamua mashindano hayo yafanyike Zanzibar mwakani baada ya
mwaka huu kufanyika Bunjumbura Burundi hivi karibuni ambapo wenyeji Burundi
walishinda nafasi ya kwanza na Zanzibar ikashinda nafasi ya pili.
“Baada ya kukutana shirikisho letu, tumeamua mwakani Zanzibar
awe mwenyeji wa mashindano, ambapo yafanyike kabla ya mwezi wa tatu mwakani”.
Alisema Mbalambula.
Katika mashindano 10 yaliopita Zanzibar imeshawahi kuwa
mwenyeji katika mashindano hayo ambapo iliwahi kuandaa mwaka 2008 na mwaka
2013, mwakani itakuwa ni mwaka wa tatu kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa mashindano
hayo makubwa ya Judo Afrika Mashariki na Kati.
No comments:
Post a Comment