Friday 22 April 2016

ALEXIS SANCHEZ AIPATIA ARSENAL 2-0

Washika bunduki wa London Arsenal wakicheza katika uwanja wao wa Emirate wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich Albion.

 

Katika mchezo huo mshambuliaji Alexis Sanchez ndie alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kuzipasia nyavu mara mbili alianza kufunga goli la kwanza  katika dakika ya sita  6, kisha akafunga goli la pili kwa mpira wa adhabu katika dakika ya 38.

 

Katika mchezo huo timu ya Arsenal iliutawala kwa asilimia 71, huku West Brom wao waliutawala kwa asilimia 29.

 Kwa ushindi huo vijana wa Profesa Arsenal Wenger, wanajiweka katika nafasi nzuri ya kuwa kwenye nne bora baada ya kujikusanyia alama 63 katika michezo 34 waliyocheza.

Arsenal wamesaliwa na michezo minne mkononi kabla ya kumalizika kwa ligi kuu England msimu huu.

No comments: