Katika mchezo huo Sadik
Habib alianza kuiandikia Mafunzo bao la kwanza mnamo dakika ya 36, bao ambalo
lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.
Mafunzo walijipatia bao
la pili katika dakika ya 76 kupitia mchezai
aliyetokea bench Rashid Abdalla ambae amechukua nafasi ya Kheir Salum,
na mchezo kumalizika kwa Mafunzo kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya
Mtende.
Kocha wa timu ya Mtende
Abrahman Mussa, amezungumza na SALMA
SPORT’S MEDIA na amesema mchezo ulikuwa mzuri lakini matokeo yao bado sio
mazuri.
“Mchezo mzuri lakini matokeo yetu bado sio
mazuri,sasa hivi tunamatatizo kwa upande wa wachezaji, wachezaji wetu sasa hivi
kidogo wameondoka, kwa hiyo hapa tunakuja
tuna wachezaji 10, 12, moja kati yam abo ambayo yanasababisha tusifanye vizuri,
kama wachezaji wetu watarudi basi tutafanya vizuri”. Alisema kocha Abrahman.
Aidha kocha wa timu ya
Mafunzo Moh’d Shaaban Kachumbar, amesesma wamekuja washinde ili wakamate nafasi
za juu na waingie katika hatua ya nne bora.
“Tumekuja tushinde
mechi ya leo ili tukamate nafasi ya pili tuingie hatua ya nne bora,
tukibahatika kuingia hatua ya nne bora kwa timu yangu mm ninavyoijua Mafunzona
mwalimu wetu mkuu alokuwepo basi tunahakikisha kupigana kuchukua ubingwa wa Zanzibar”.
Alisema Kachumbar.
Matokeo hayo
yameipandisha Mafunzo hadi nafasi ya tatu (3) wakiwa na alama 35, na Mtende wanashika
mkia wakiwa na alama kumi (10).
No comments:
Post a Comment