Sunday 28 February 2016

HILI NDIYO JIBU LA SAMATTA BAADA YA KUULIZWA ANAOA LINI

Siku chache zilizopita, mtangazaji wa kitanzania Salim Kike anaefanya kazi kwenye shirika la utangazaji la BBC alisafiri kutoka jijini London England hadi Genk, Belgium kufanya mahojiano na mchezaji wa Bongo Mbwana Samatta ambapo walizungumza mambo kibao kuhusu maisha binafsi ya nyota huyo.
Kikeke: Nani anakupikia misosi huku?
Samatta: Mimi napika mwenyewe
Kikeke: Unapika mwenye ugali?
Samatta: huku hata unga wenyewe sijawahi kuuona
Kikeke: Ungeniambia ningekuletea unga kutoka London
Samatta: London kuna Unga?
Kikeke: Kwahiyo unapika?
Samatta: Napika wali maharage, tambi. Rahisi sana ni tambi.
Kikeke: Nani kakufundisha kupika tambi Samatta
Samatta: Inategemea na maisha niliyokulia. Nimekua kwenye maisha ya makaka na mashemeji kwahiyo kilasiku walikuwa wanapika.

No comments: