Hatimaye ubingwa wa La Liga umedhihirika hauwezi kwenda Santiago Bernabeu kwa mwaka wa 3 mfululizo sasa baada ya Real Madrid kupokea kipigo kutoka mahasimu wao Atletico Madrid.
Vijana wa Zinedine Zidane wanaweza kujikuta wapo nyuma ya Barcelona kwa pointi 12 baada ya wikiendi hii, ikiwa Blaugrana wataifunga Sevilla kesho.
Tofauti hii ya pointi kati ya Madrid na mahasimu wao imekuja kutokana na Madrid kuwa na rekodi mbovu dhidi ya timu za Top 10 ya La Liga.
Los Blancos wamefanikiwa kupata pointi moja tu kati ya 15 walizotakiwa kupata dhidi ya vilabu vitano vikubwa. Walifungwa ugenini na Villareal na Sevilla, nyumbani wakakubali kipigo dhidi ya Barcelona Na Atletico. Pointi moja waliyopata ilitokana na sare ya 1-1 dhidi ya Atletico Madrid @VicenteCalderon.
Hivyo wamepoteza pointi 14 dhidi ya vilabu vikubwa, Madrid bado wana kizingiti cha kucheza Nou Camp vs Barcelona na kuwakaribisha Sevilla na Villareal @SantiagoBernabeu.
Hivyo wamepoteza pointi 14 dhidi ya vilabu vikubwa, Madrid bado wana kizingiti cha kucheza Nou Camp vs Barcelona na kuwakaribisha Sevilla na Villareal @SantiagoBernabeu.
Takwimu za Barcelona dhidi ya timu hizo – wamepata pointi 12 kati ya 15. Pointi 11 zaidi ya Madrid, na wanaweza kuziongeza kufikia 14 ikiwa watashinda kesho dhidi ya Sevilla.
No comments:
Post a Comment