Manchester City wamefanikiwa kufuzu kucheza robo fainali ya
michuano ya Champions League kwa mara ya
kwanza licha ya kutoka sulusu kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Dynamo
Kiev jana usiku.
City ilishinda kwa bao 3-1 kwenye mchezo wa awali, walianza
vyema mchezo huo lakini wakajikuta wakiwakosa walinzi wao nguzo wa kati Vincent
Kompany na Nicolas Otamendi dakika za mapema baada ya kuanza kwa mchezo huo kutokana na kupata
majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo.
Hadi kipindi cha kwanza inamalizika hakuna timu ambayo
ilikuwa imepiga hata shuti moja on target. Jesus Navas alipiga shuti ambalo
liligonga mwamba wakati shuti la Yaya Toure likiokolewa na mlinda mlango wakati
wa kipindi cha pili.
Draw kwa ajili ya hatua ya robo fainali (nane bora) itapangwa
Ijumaa baada ya michezo ya leo kuwa imemalizika (Bayern vs Juventus na
Barcelona vs Arsenal)
Pellegrini amesema Kompany anaweza kuwa nje ya uwanja kwa
kipindi kisichopungua miezi minne, kwahiyo City inasubiri kuona kama Otamendi
anaweza kurejea uwanjani kwa ajili ya mechi za Premier League dhidi ya Manchester
United siku ya Jumapili.
Rekodi zilizowekwa na Man City
•Manchester City ni timu ya saba nyingine tofauti kuingia
robo fainali ya Champions League kutoka England baada ya Arsenal, Tottenham,
Leeds, Liverpool, Manchester United pamoja na Chelsea tangu mwaka 1992
•Man City wameweka rekodi ya kucheza mechi 10 bila kuruhusu
nyavu zao kutikiswa kwenye michuano hiyo ya Ulaya mara ya mwisho ilikuwa ni
December 2014 dhidi ya Roma.
•Mchezo wa jana usiku ulikuwa ni wa pili Manchesyer City
inacheza dakika 90 bila kupata bao kwenye michuano ya Champiuons League ndani
ya uwanja wa Etihad
•City waliweza kupiga shuti moja tu on target wkati wa
mchezo, shuti hilo lilipigwa dakika ya 73 kipindi cha pili.
Shaffih Dauda.
No comments:
Post a Comment