Friday 1 April 2016

Emmanuel Eboue aangukia kisu cha FIFA


Kamati ya nidhamu ya FIFA imetoa onyo kali kwa Emmanuel Eboue na kumtishia adhabuendapo atashindwa kulipa deni analodaiwa na meneja wake.

Kamati hiyo imesema kwamba itaweza kumfungia Eboue kwa mwaka mmoja kwa kushindwa kumlipa meneja wake aliyefanya makubaliano naye kuanzia tarehe 9 Machi hadi mwishoni mwa msimu huu.

Sebastien Boisseau ambaye ni meneja wa nyota huyo wa Ivory Coast, aliwasilisha kesi hiyo ya deni lake analomdai Eboue kwa FIFA.

Hapo awali, kamati hiyo pia iliwahi kumtoza Eboue faini ya fedha Franc 30,000 baada ya kushindwa kumlipa meneja wake licha ya kupewa muda wa siku 120.

No comments: