Friday, 1 April 2016

Infantino aunga mkono Argentina na Uruguay kuandaa kombel la dunia 2030


Rais wa FIFA Gianni Infantino, ameunga mkono pendekezo la kuandaa kombe la dunia la mwaka 2030 nchini Argentina na Uruguay.

Infantino alitoa maelezo hayo wakati za ziara yake aliyoitekeleza kwenye makao makuu ya shirikisho la soka la Amerika ya Kusini CONMEBOL nchini Paraguay.

Katika maelezo yake, Infantino alibainisha kuunga mkono mpango wa maandalizi ya kombe la dunia kufanyika katika nchi zaidi ya moja.


Hapo awali, kombe la dunia la mwaka 2002 pia liliwahi kufanyika katika nchi mbili ambazo ni Japan na Korea Kusini barani Asia.

No comments: