Friday 20 May 2016

JKU YABANWA MBAVU NA BOY’S LIGI KUU ZANZIBAR



Vinara wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja  timu ya Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar JKU imeshindwa kutamba baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana walipocheza na Jang’ombe boy’s.

Mtanange huo uliovurumishwa ndani ya dimba la Amani, timu hizo zilionesha upinzani kwani kila timu ilitaka kuondoka na alama tatu katika mechi hiyo.

Licha ya kuonesha kiwango kizuri siku ya leo,Jang’ombe boy’s kwa sasa imeondoa matumaini ya kuingia nne bora ambapo leo ulikuwa ni mchezo wake wa 22, wakiwa wana alama 26, na wapo nafasi ya kumi kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Wakati JKU wao ndio vinara wa ligi hiyo wakiwa wameshuka dimbani mara 22 na wana alama 51, wakitofautiana kwa alama 12 na timu inayoshika nafasi ya pili amabyo ni timu ya Mafunzo.

No comments: