Aliyekuwa winga wa timu ya Ufaransa David Ginola anaendelea kupata afueni hospitalini mjini Monaco baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 49 ambaye aliwahi kuichezea Newcastle,Tottenham,Aston Villa na
ambaye alijiuzulu mwaka 2002 alianguka na kuzirai kusini mwa Ufaransa.
Daktari aliyemfanyia
upasuaji huo amesema kuwa Ginola alinusurika kifo.
Ujumbe wa Twitter
kutoka kwa nyota huyo wa zamani ulisema: Walimwengu hamjambo,sikulala
vizuri.Niko salama ,ijapokuwa nataka kupumzika kiasi.
David alicheza katika
mechi ya hisani .Lakini ghafla akaanguka na kuzirai huku watu wakidhani ilikuwa
mzaha lakini baada ya dakika mbili wakabaini mchezaji huyo yupo
hatarani,alisema Gilles Dreyfus,profesa wa upasuaji katika hospitali ya kukabiliana
na magonjwa ya moyo huko Monaco.
bbc.
No comments:
Post a Comment