Mwanaspoti Servet Tazegül apeperusha bendera ya Uturuki kwenye mashindano ya taekwondo barani Ulaya
Servet Tazegül ambaye
ni mshiriki wa taekwondo, aliibuka mshindi barani Ulaya kwenye mashindano ya 22
ya tekwondo yaliyoandaliwa mjini Montro nchini Uswisi.
Servet Tazegül
aliyekuwa akiwakilisha Uturuki kwenye mashindano hayo ya Ulaya, alishinda
nishani ya dhahabu katika kitengo cha washiriki wa kiume wa uzani wa kilo 68.
Katika mashindano hayo,
Servet Tazegül aliwashinda Boriz Ruizi wa Andora 3-2 , Ben Haines wa Uingereza
6-2 na Viacheslav Minin wa Urusi 9-7 kwenye raundi ya pili, tatu na robo
fainali mtawalia.
Katika hatua ya nusu
fainali, Servet Tazegül alimshinda Konstantin Minin wa Urusi 15-5 na kutinga
fainali kwa kishindo ambapo alipambana na mjerumani Hamza Adnan-Karim mwenye
asili ya Turkmenistan.
Servet Tazegül aliibuka
bingwa baada ya kushinda fainali hiyo 6-5 na kuweza kunyakuwa nishani ya
dhahabu kwa mara ya 5 ikiwa ni pamoja na mwaka 2008,2010,2012 na 2014.
Kwa upande wa wanawake,
Zeliha Ağrıs wa Uturuki pia aliweza kushinda nishani ya shaba kwa washiriki wa
uzani wa kilo 53.
Zeliha Ağrıs alimshinda
Tatiana Kudashova wa Urusi 10-6 kwenye fainali ya kuwania nafasi ya tatu.
No comments:
Post a Comment