Manchester United wameshinda Kombe la FA baada ya kuwalaza Crystal Palace 2-1 katika fainali iliyochezwa uwanja wa Wembley.
Ni mara yao ya kwanza
kushinda kikombe hicho tangu 2004.
Mabao ya Manchester
United yalifungwa na Juan Mata katika dakika ya 81 na Jesse Lingard dakika ya
110.
Bao la kufutia machozi
la Crystal Palace limefungwa na Jason Puncheon dakika ya 78.
Ushindi huo ni nafuu
sana kwa meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye amekuwa akikabiliwa
na shinikizo kutokana na kutofana kwa klabu hiyo.
Kwa ushindi huo,
Manchester United wamefikia rekodi ya Arsenal kwa kushinda kombe hilo mara 12.
Akizungumza baada ya
mechi hiyo, Van Gaal alisema amefurahia sana kushinda kikombe hicho.
"Ni muhimu sana
kushindia klabu kikombe hiki, kwaa mashabiki, na mimi pia kwa sababu sasa
nimeshinda katika mataifa manne, na si mameneja wengi wamefanikiwa kufanya
hivyo," amesema Van Gaal.
No comments:
Post a Comment