Muhammad Ali alikuwa bondia kwa sababu kuna mtu aliyemuibia
baskeli yake. Alikuwa na umri wa miaka 12 wakati ule na alikuwa akiishi
Louisville katika jimbo la Kentucky akijuilikana kwa jina la Cassius Mercellus
Clay Jr.
Joe Martin, aliyekuja kuwa kocha wake baadaye, anaelezea
jinsi kijana huyo alivyokuwa akilia huku akiahidi kumtandika magumi aliyemuibia
baskeli yake pindi akimpata. Kocha huyo wa ubondia alimchukua Clay, kijana
mweusi anayetokea katika familia ya watu maskini, na kumjumuisha na watoto
wengine aliokuwa akiwafundisha.
“Alikuwa na bidii zaidi kuliko waatoto wote wengine niliokuwa
nikiwasimamia,” anasema Joe Martin.
Ingawa Clay wakati ule hakuwa na nguvu ya kuvurumisha
masumbwi, alikuwa mwepesi wa kuranda randa kupita kiasi. Mnamo mwaka 1960,
akiwa na umri wa miaka 18, alishinda katika pambano la ndondi la michezo ya
Olympiki mjini Rome, Italia. Medali yake ya dhahabu inasemekana aliitupa ndani
ya Mto Ohio kwa sababu alikasirishwa na jinsi watu weusi wanavyobaguliwa nchini
mwake.
Cassius Clay alikamilisha michuano ya wasiolipwa baada ya
kuibuka na ushindi mara 100 katika jumla ya mapambano 108 aliyopigana.
Wafanyabiashara 11 wa Kizungu kutoka Louisville walishirikiana ili kumfungulia
njia Cassius Clay ya kuingia katika ulingo ya mabondia wa kulipwa.
Bondia huyo mwenye kipaji alikuwa akitajikana pia kuwa ni mtu
aliyekuwa na majivuno na mdomo mpana. Kabla ya mapambano yake, Cassius Clay
daima alikuwa akijinata kuwa yeye “ndie mbabe wa wababe na mzuri kuliko
mabondia wote na kuwakejeli wapinzani wake.
Katika pambano lake la kwanza la kuwania ubingwa wa dunia
Februari 1964 dhidi ya mtetezi wa taji hilo, Sonny Liston, Clay hakuwa
akijulikana ni nani na watu waliamini angeshindwa tu. Lakini baada ya raundi ya
sita, Liston aliungama. “Mie ndie mbabe,” alinguruma Cassius Clay kupitia
kikuza sauti.
Mwaka huo huo, alisilimu na kujiunga na kundi la Nation of
Islam lililokuwa likiongozwa wakati huo mwanaharakati wa haki wa Wamarekani
Weusi, Malcolm X. Akabadilisha jina la Cassius Clay na kujiita wakati huo huo
Muhammad Ali
Muhammad Ali hakuwa bondia tu, alikuwa mwanaharakati pia.
Alipinga vita vya Marekani nchini Vietnam na alikataa kutekeleza sheria ya
kutumikia jeshi. Mnamo mwaka 1967, akapokonywa sio tu leseni yake ya ubondia,
bali pia alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela, ingawa baadaye bondia huyo
wa aina pekee aliachiwa kwa dhamana.
Wasanii na wasomi mfano wa Richard Burton na Henry Fonda au
mwandishi vitabu Truman Capote wakampigania mpaka Muhammad Ali akaruhusiwa tena
kurejea ulingoni baada ya kulazimika kukaa nje kwa miaka mitatu.
Machi 8, 1971 Muhammad Ali aliteremka ulingoni Madison Square
Garden mjini New York kwa kile kilichotaajwa “kuwa pambano la ndondi la karne”
dhidi ya bingwa wa wakati ule, Joe Frazier. Lilikuwa pambano kati ya mafahali
wawili, kati ya mpinzani na yule aliyekuwa akiangaliwa kama mwakilishi wa
mtindo wa maisha wa Kimarekani. Katika pambano hilo la kusisimua la zaidi ya
raundi 15, Frazier akashinda kwa pointi. Ali akalazimika kwa mara ya kwanza
katika maisha yake ya ubondia kunusa jamvi.
Yakafuata mapambano mengine ya kusisimua mfano wa lile la
mjini Kinshasa dhidi ya George Foreman mnamo mwaka 1974, ambapo Muhammad Ali
anasema “aliranda mfano wa kipepeo na kuuma kama nyuki”
Muhammad Ali alilipiza kisasi dhidi ya Joe Frazier mwaka 1975
na kumlazimisha kusalimu amri mnamo rauni ya 14. Mohammed Ali alistaafu
mwishoni mwa mwaka 1981 baada ya kuranda kwa karibu miaka 40.
Wakati huo tayari alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya
Parkinson. Licha ya maradhi hayo, Muhammad Ali ndiye aliyewasha mwenge wa
Olimpiki huko Atlanta mnamo mwaka 1996 na kuusisimua ulimwengu mzima. Mwaka
1999 aliteuliwa na kamati kuu ya michezo ya Olimpiki kuwa “mwanaspoti bora wa
karne.”
Mpinzani wake wa zamani George Foreman amegeuka hivi sasa
kuwa rafiki yake mkubwa na kuungama “Muhammad Ali ndie bingwa wa mabingwa.”
Mpaka leo june 4 2016. Muhhamad Ali anapoteza maisha ndie
mwanamasumbwi mstaafu kutoka nchini Marekani. aliepata kuwa bingwa wa uzito wa
juu mara tatu.
JE, WATU WANASEMAJE KUHUSU MUHAMMAD ALI?
Aliyekuwa mwanamasumbwi George Foreman aliyewahi kupambana na
Mohammad Ali katika mechi iliofanyika Zaire (Sasa DRC) .
George Foreman: Aliyekuwa mwanamasumbwi George Foreman
aliyewahi kupambana na Mohammed Ali katika mechi iliofanyika Zaire (Sasa DRC)
kabla ya Ali kuibuka mshindi, anasema kuwa Mohammed Ali alikuwa na ushawishi wa
kukufanya akupende. Iwapo usingempenda angekufanyia vituko zaidi ndio uweze
kumchukia zaidi.
Floyd Mayweather Jr: Leo moyo wangu unanung’unika kwa
kumpoteza mwanzilishi, bondia hodari, bingwa na shujaa kwa vyovyote vile.
Hakuna siku niliingia katka ulingo wa ndondi bila kumkumbuka , alisema katika
mtandao wa instagram. Ucheshi, uzuri wako na vinginevyo ndio vitu
tutakavyovienzi.
Odesa Grady Clay: Kila mara nilihisi Mungu alimfanya Muhammad
kuwa mtu muhimu, lakini sijui kwa nini Mungu alinichagua mie kumbeba mwana
huyu, wakati alipokuwa mtoto hakuweza kutulia, alitembea na kuzungumza na
kufanya kila kitu wakati wake. Akili yake ilikuwa kama upepo unaovuma na
kueleka kila sehemu.
Rahman Ali: Nduguye Mohammed Ali anasema kuwa marehemu
alikuwa akimtaka amrushie mawe, nilidhani ameshikwa na wazimu, lakini mawe hayo
angeyahepa yasimpige…sikuweza kumpiga.
Malcom X: Ndio mwanamichezo hodari mweusi niliyewahi kumjua
na ana umuhimu mkubwa kwa watu wake. Kwa sababu mabilioni ya watu kutoka
Afrika, Asia na Arabia wanakupenda lazima ujue majukumu yako.
Jesse Jackson:Walikataa kusikiliza ushuhuda wake kuhusu dini
yake. Walijaribu kumnyanyasa, walijaribu kumuathiri kimwili na kiakili
Je,nini kilimshinikiza Ali kujiunga na ndondi?
Muhammad Ali alijiunga na masumbwi kwa bahati.
Ali aliyekuwa na umri wa miaka 12 alikuwa na marafikize
wakitafuta peremende na porp corns za bure.
Na alipogundua kwamba baiskeli yake imeibwa aliagizwa kwende
chini ya nyumba aliyokuwepo katika taasisi ya mafunzo ya Columbia ambapo afisa
wa polisi Joe Martin alikuwa akisimamia mpango wa ndondi.
Martin alimwelezea Ali kwamba angeanza kunoa ngumi zake kwa
kujifunza ndondi kabla ya kumtafuta mwizi huyo.
Kwa haraka alijua vile ambavyo angejichukulia na alipofika
umri wa miaka 18 alikuwa ameshinda dhahabu ya Olimpiki mjini Rome.
No comments:
Post a Comment