Friday 26 February 2016

CHUONI YALAZIMISHWA SARE DAKIKA ZA MAJERUHI.


Timu ya chuoni jana imetoka sare ya bao moja kwa moja walipocheza na Miembeni katika ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja.

Mchezo huo uliosukumwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi 10 za jioni, timu zote zilicheza mpira kwa kwa kusaka bao kutokana na kufanya mashambulizi mara kwa mara.

Timu ya Chuoni ilizidi kufanya mashambulizi ya kushtukiza na ndipo mchezaji Mshamba Mcha Faki akaipatia timu yake ya Chuoni bao la kuongoza katika dakika ya 33.
Na hadi timi zinakwenda mapumziko chuoni walikuwa mbele kwa bao moja.

Katika kipindi cha pili, wachezaji wa Miembeni walirudi uwanjani kwa kasi kwa kutaka kurudisha bao hilo, na hatimaye mchezaji Ramadhan Hamza Kidilu akawanyanyua mashabikimwake baada ya kurudisha bao hilo katika dakika za nyongeza za mchezo huo.


Na mtanange huo ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Baada ya matokeo hayo timu ya Miemeni sasa wapo nafasi ya tano (5) na alama (23), huku chuoni wao wakiwa nafasi ya tisa (9) na alama kumi na nane (18).

No comments: