Wednesday 13 April 2016

GOLDEN STATE WARRIORS YAWEKA REKODI MPYA YA USHINDI NBA



Mabingwa watetezi wa taji la ligi kuu ya mpira wa kikapu ya NBA nchini Marekani Golden State Warriors, wamevunja rekodi ya msruru wa ushindi wa mechi nyingi zaidi ndani ya msimu mmoja.

Golden State Warriors walishinda mechi yao ya 72 baada ya kuipindua San Antonio Spurs kwa vikapu 92-86 kwenye mechi iliyochezwa hapo jana.

Kufuatia ushindi huo, Golden State Warriors iliweza kuvunja rekodi ya ushindi wa mechi nyingi zaidi ndani ya msimu mmoja wa NBA iliyokuwa ikishikiliwa na Chicago Bulls.


Katika mechi hiyo dhidi ya San Antonio Spurs, nyota wa Golden State Warriors Stephen Curry aliibeba timu yake kwa kufunga jumla ya vikapu 37.

No comments: