Tuesday 5 April 2016

KVZ YABANWA MBAVU NA POLISI.



Timu ya Kikosi cha Valantia  Zanzibar  KVZ  leo imebanwa mbavu na Polisi  baada ya kutoka sare ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa ndani ya dimba la Amani majira ya saa kumi za jioni.

Katika mchezo huo timu ya Polisi ilionekana kucheza vyema licha ya kuonekana kusuasua tangu kuanza kwa ligi hiyo wakiwa wameshinda mchezo mmoja tu katika michezo 17 waliyocheza.

SALMA SPORTS MEDIA ilizungumza na kocha wa timu ya KVZ Abdulghani Musoma amesema kuwa hawakucheza vizuri na hawakumiliki mpira kwa kujenga mashambulizi lakini wangeweza kumiliki mpira vizuri kwa kupeana pasi vizuri na kutafuta nafasi za kupenyeza wangeweza kushinda, alisema Musoma.

Kwa upande wa kocha wa timu ya Polisi Ali Suleiman Mtuli amesema kuwa, hali bado ni tete kwa sababu bado hawajafanya vizuri sasa wanajitahidi kutengeneza timu lakini hali hii bado haijaondoka, alisema Mtuli.

Kwa matokeo hayo timu ya KVZ bado wapo nafasi ya pili na wamefikisha alama 30, lakin Polisi wao wakiwa nafasi ya pili kutoka mkiani na alama tisa (9).

 

No comments: