Saturday 27 February 2016

VIONGOZI WA SOKA WAJALINI WACHEZAJI WENU.




Soka la Tanzania limesemwa kua ni  shida kukua kutokana na kutokuwepo kwa mpangalio mzuri wa kuwezesha wachezaji na soka lenyewe ili kulikuza.

Kauli hiyo imetolewa na Yunus Dady wa timu ya “Bhulyanhulu” ya Shinyanga  inayo cheza  daraja la pili kugombania kufuzu ligi daraja la kwanza wakati alipokua akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA juu ya mtazamo wake kwa soka la Tanziania.

Mengi  ameyaongea mchezaji huyo na katika maongeziyetu ilikua kama ifuatavyo:-
Salma Hassan: unalizungumziaje soka la Tanzania  kwa ujumla?

Dady: mpira wa Tanzania  kiufupi ni mgumu na wanaofanya uwe mgumu ni baadhi ya viongozi.
Salma Hassan: oky sawa , kivipi unakua mgumu au awo viongozi wanaufanya vipi kua mgumu?

Dady: kwamfano utakuta mtu anacheza timu kubwa hapa nchini  lakini inafikia hatua mchezaji miez mitatu (3) mapaka mine(4)hajapewa  mshahara wake hivi unategemea mchezaji kama huyu anaweza kumentain pafomance yake wakati maisha yetu haya tunayajua wenyewe ! lakini ni tofauti kabisa na wenzetu wa Ulaya wanajali , wanathamini na wanajua kuvienzi vipaji na wachezaji.

Salma Hassna: kama hali ndio hiyo uliyoieleza ni kweli mchezaji anaweza kurudi nyuma kutokana na mazingira mabovu kama hayo kulinganisha na maisha ya wengi hapa nchini ni “duni” kwa uwoni wako nini kifanyike ili kuinua soka letu ?

Dady: kitu cha kwanza viongozi waache ubabaishaji, kwa sababu Tanzania na timu zake wanavipaji vingi sana  lakini viongozi wanaviua wenyewe  eti  huwez kucheza Primier ligi  mpaka upate mtu wa kukusimamia na awe anakupigia debe ucheze hata uwe na kipaji gani lazima awepo mtu awe na sauti juu yako wa kukusimamaia la sihivyo huwez kupata nafasi ya kucheza na utaishia patupu! na mifano ipo mingi, sasa hivi kuna watu wapo vijijini wanauwezo mkubwa lakini ndio hivyo wanaachwa na pia Sponser (wadhamini )hawana sasa watafanya nini.

Yunus Dady amemalizia kwa kutoa wito kwa viongozi wote wa soka nchini kua makini na kujali kipaji na uwezo wa mchezaji lakini pia kuzingatia maslahi ya mchezaji wenyewe,wawezeshwe ili nao wapate moyo kwa kucheza kwa bidii na hatimae kukuza soka letu hapa nchini.


Dady ni mchezaji machachari  nae valia  jez nambari  5 mgongozi na uwanjani anachezea  beki wakati nambari tano 5.

1 comment:

Unknown said...

ni kweli kabisa viongozi huwa wanajali maslahi yao zaidi