Friday 25 March 2016

KAMPENI “FICHUA VIPAJI”



Anaandika Salma Hassan

Alievaa T.shirt nyeupe ni Yassin Wito na mwenzake Abuu Linco  wa timu ya Shein Rangers kutoka Zanzibar wakiwa na furaha kubwa baada ya kutwaa ubingwa katika ligi ijuulikanayo “VESPER LIGI ”huko Nungwi  nje kidogo na mji wa Zanzibar.

Ligi hii ilianzishwa maalum kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana na ni ligi iliyochezwa na vijana wenye umri  wa chini ya miaka 15.

Serikali na wahisani nchini kutokana na maoni ya wananchi wapenda michezo, wengi wao wameshauri na kupendekeza kuwa, ili kukuza soka nchini Zanzibari ni lazima kuwepo na mashindani kama haya madogomadogo kwa lengo la kuibua vipaji vya watoto.

Inaaminika kua Zanzibar kuna vipaji vingi sana lakini vinashindwa kuonekana kutokana na kutokuwepo kwa mbinu mbadala kama hizi za hatimae huishia mitaani tu.






No comments: