Wednesday 30 March 2016

MATUMAINI YA KUCHEZA LIGI KUU YAYEYUKA



Matumaini ya timu ya Mkungu Malofa kucheza ligi kuu ya Zanzibar hapo mwakani leo yameyeyuka baada ya kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa timu isiyotabirika ya Majimaji katika mchezo uliochezwa leo katika uwanja wa Gombani.

Mchezo huo ambao Mkungu Malofa ingeshinda ingeungana Wawi Star kuelekea ligi kuu hapo mwakani lakini kile ambacho kilitarajiwa na wengi kimetoweka jioni hii baada ya Maji maji kuondoka na ushindi huo na kupeleka majonzi katika mitaa ya Mkungu malofa.

Alikuwa ni Khamis Hamza wa Maji Maji aliyeanza kupeleka majonzi kwa timu ya Mkungu Malofa katika dakika ya 20 ya mchezo aliyemimina majaro kutoka upande wa kushoto na mlinzi Khamis Ali Hassan wa M/Malofa akijikuta akiuingiza mwenyewe mpira huo ukipishana na golkipa Aziz Ali.

Hadi Mapimziko Maji maji 1 na Mkungu Malofa bila.

Katika dakika ya 59 ya Mchezo Massoud wa Maji maji alifanikiwa kuiandikia timu yake bao la pili.

Hata hivyo mwamuzi wa mchezo huo Moh`d Seif aliwatoa nje kwa kadi nyekundu wachezaji Nassor Moh`d Nassor wa Mkungu Malofa na Bakar Said wa Maji maji kutokana na kuonyeshana ubabe kiwanjani hapo.

Dakika 1 kuelekea kumalizika kwa mchezo huo Mussa Ali wa Mkungu Malofa aliweza kuipatia timu yake bao la kujifariji.

Kwa matokeo hayo timu ya Maji maji ambayo imemaliza michezo yake yote imefikisha alama 7  na kushika nafasi ya 2 huku timu Mkungu Malofa wakiishia na alama 5.


Kesho ndiyo kesho pale michezo miwili itakapo pigwa kwa wakati mmoja, Chuo Bassra yenye alama 6 watakuwa na Danger Boys yenye alama 4 katika uwanja wa Gombani, huku New Star yenye alama 4 ikizisaka alama tatu kutoka kwa Wawi Star yenye alama 10 kwenye uwanja wa Ngerengere.

No comments: