Wednesday 30 March 2016

FICHUA VIPAJI YAPENYA KATIKA VISIWA VYA KIJANI.


Camera ya SALMA SPORT’SMEDIA jana ilifanikiwa kunasa kikosi cha timu ya Ng’ambwa FC Junior Chake Chake.

Safari haikua ndogo mwanamichezo wetu Is-haq Muhammed alitumia kila liwezekanalo kuitafuta timu hii  ili  kuzungumza nawo na  kujua nini hasa malengo yao katika usakataji wa kabumbu.

Mengi sana walizungumza wachezaji hawa lakini ukiyakusanya na kuyatazama kwa undani utakugundua yote yanalingana, ni kwamba lengo ni kukuza kiwango cha soka nchini na kukua wao wenyewe.

Malengo haya yapo na ni yakawaida kwa timu nyingi lakini natujiulize hivi kweli wanachokiwaza ndicho kitakachotokea?

Jibu la suala hili utakua nalo wewe kisha chukua hatua kama ni mdau wa michezo kwa shabaha ya  kuwainua vijana wetu na kuinua taifa letu.


Kwanini tusisifikane ulimwenguni kote wakati uwezo tunao, nini hasa tatizo letu. Mdau tumekuletea hili tafakari kisha kuchukua hatua vipaji ndio hivyo vinazurura mitaani.

No comments: