Tuesday 26 April 2016

BOY’S YAWAKOMALIA KVZ.

Timu ya Kikosi cha Valantia Zanzibar KVZ  imeshindwa kutamba katika mchezo wa ligi kuu ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Jang’ombe boy’s mchezo ambao umesukumwa ndani ya uwanja wa Amani mjini Unguja.


Licha ya mchezo huo kuchezwa katika hali ya mvua lakini boy’s walijipatia bao la mapema lililofungwa na Abrahman Othman katika dakika ya 16, ambalo lilikuwa ni bao pekee katika mchezo huo lililoweza kuwapatia boy’s alama tatu  za mchezo.

Katika dakika ya 74 mlinda mlango wa Jang’ombe boy’s Ali Yussuf alimfanyia faulu mchezaji wa KVZ Nassir Bakar ndani ya boks, na ndipomwamuzi wa mtanange huo aliamuru kupigwa kwa mkwaju wa penalt, lakini mchezaji wa KVZ Suleiman Ali aliikosa penalt hiyo baada ya mlinda mlango Nassir kuutoa mpira huo.

Akizungumza na SALMA SPORT’S MEDIA kocha wa Jang’ombe boy’s Issa Othman Amasha ambae wameibuka na ushindi huo licha ya kushinda lakini  amesema kuwa tatizo la ufungaji bado lipo kwa wachezaji wake. “Tatizo la ufungaji bado lipo lakini sasa, leo siwezi kulaumu sana kwa sababu mpira wenyewew ulikuwa ni wa mvua”. Alisema kocha Amasha.

Lakini kocha wa timu ya KVZ Othman Hassan King, amesema hali ya hewa ndio iliyosababisha mechi kuwa ngumu kwao.

“Mechi ya leo kutokana na hali ya hewa, kidogo imesababisha mechi hii kubadilika kutokana na hali ya hewa, na hali ya hewa ndiyo iliyosababisha kuleta ugumu katika timu yangu”. Alisema kocha King.

KVZ bado wamesalia nafasi yao ya pili wakiwa na  alama 33, na Jang’ombe bpy’s sasa wapo nafasi ya kumi 10 na alama 22.

 

No comments: