Monday 4 April 2016

Manchester United yapata ushindi wa nyumbani


Timu ya Manchester United ilijitosa kwenye uga wa Old Trafford kupambana na Evertonkwenye mechi ya ligi kuu ya soka ya EPL nchini Uingereza.
Wenyeji Manchester United walileta faraja mbele ya mashabiki wao kwa kujihakikishia pointi 3 dhidi ya wageni Everton.
Licha ya kuwa na wakati mgumu kwenye mchuano huo, Manchester United ilifanikiwa kupata goli moja la pekee lililofungwa na Anthony Martial katika dakika ya 54.
Ushindi huo wa 1-0 uliiletea Manchester United pointi 3 na kuiwezesha kukaa katika nafasi ya 5 ikiwa na jumla ya pointi 53.

No comments: